Semina zimesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu/ tawi la wilaya ya Kamiit kwa ushiriki wa karibu wanafunzi elfu saba.
Hafla ya kufunga semina imehudhuriwa na wanafunzi pamoja na wazazi wao, imepambwa na vipengele tofauti.
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema “Maahadi ya semina za Qur’ani imehitimisha semina za majira ya kiangazi katika mkoa wa Misaan na viunga vyake, jumla ya washiriki walikuwa 7000 na zimedumu kwa muda wa siku 40”.
Akaongeza kuwa “Wanafunzi wamesoma mambo tofauti wakati wa semina hizo, wamesoma Fiqhi, Aqida, Akhlaq, Sira ya Ahlulbait (a.s), hukumu za usomaji wa Qur’ani sambamba na kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s)”.
Akabainisha kuwa “Semina zinalenga kufundisha utamaduni wa Ahlulbait (a.s) na elimu yao, kusoma hukumu za Qur’ani na kuhifadhi” akaongeza kuwa “Semina hizi ni sehemu ya kupambana na changamoto za vijana wanazokumbana nazo kwa sasa”.