Atabatu Abbasiyya imefanya kikao maalum cha kutangaza majina ya washindi wa mashindani yaliyofanywa katika wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.
Kikao kimefanywa katika jengo la Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya, kimehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Jawadi Hasanawi, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya marais wa vitengo na viongozi wengine.
Wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili, imepambwa na mashindano tofauti, kulikuwa na shindano la mashairi, shindano la kisa kifupi, shindano la kupiga picha za fotograf kwa kutumia simu na mengineyo.
Atabatu Abbasiyya imefanya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili, chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kulea mtu na umma).
Atabatu Abbasiyya kupitia wiki ya Imamu huelezea elimu ya Ahlulbait (a.s) na historia yao katika kupambana na changamoto, sambamba na kubainisha nafasi yao (a.s) katika kuondoa shubha na fikra potofu.