Kikao maalum cha kutangaza majina ya washindi kimefanywa katika majmaa Al-Ameed chini ya Ataba tukufu, na kuhudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, viongozi wa idara, marais wa vitengo na viongozi wengine.
Mada za shindano zilihusu ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu na matukio ya Ataba tukufu za Iraq, limesimamiwa na kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya.
Ataba tukufu iliandaa zawadi za washindi kumi wa mwanzo.
Yafuatayo ni majina ya washindi:
- 1- Zainabu Muhammad Mussawi.
- 2- Khalidi Rahim.
- 3- Nadhiri Ali.
- 4- Sajjaad Muhammad Qassim.
- 5- Hassan Khalidi.
- 6- Mustwafa Muhammad Quraishi.
- 7- Ali Ahmadi.
- 8- Ahmadi Rahmaan Saidi.
- 9- Zainabu Majidi.
- 10- Hussein Jabaar.
Zawadi zimekabidhiwa na makamo rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, Dokta Haidari Aaraji.
Atabatu Abbasiyya inafanya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kulea mtu na umma).