Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha kongamano la Imamu Hujjat Almuntadhir (a.f) miongoni mwa ratiba za wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.
Kongamano hilo limehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, makamo wake Muhandisi Abbasi Mussa, viongozi mbalimbali na watu wengine wengi.
Mjumbe wa kamati ya kongamano Dokta Ali Idani amesema “Kamati ya kuhuisha turathi imekamilisha shughuli za kongamano la Imamu Hujjat (a.f) kupitia ratiba ya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaongeza kuwa “Kikao kimeshuhudia uwasilishwaji wa tafiti (5) zilizofuatiliwa kwa karibu na kuibua mijadala ya kielimu kutoka kwa wahudhuriaji”.
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Imamu Hujjat (a.f) katika tamko lao la ufunguzi wamesema kuwa; walipokea tafiti kumi na tisa za kielimu kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye kongamano hilo.
Mwishoni mwa kongamano katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, wajumbe wa kamati kuu Sayyid Liith Mussawi na Sayyid Kadhim, wamegawa zawadi kwa watafiti walioshiriki kwenye kongamano hilo.
Atabatu Abbasiyya imefanya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kulea mtu na umma).