Ugeni unaoshiriki kwenye wiki ya Imamu umesema: Madhumuni ya wiki ya Imamu yameakisi falsafa ya maisha na undani wa Aqida.

Ugeni unaoshiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili umesema kuwa, madhumuni ya wiki ya Imamu yameakisi falsafa ya maisha na undani wa Aqida.

Hayo yapo katika ujumbe uliotolewa na Shekhe Mustwafa Misri Al-Aamiliy kwa niaba ya ugeni huo, wakati wa shughuli za kufunga wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.

Akasema: “Wiki ya Imamu imeshuhudia kumbukumbu ya matukio matatu makubwa, ambayo ni Idul-Ghadiir, Mubahala na sadaka ya pete, kila moja kati ya matukio hayo linamafundisho ya kiaqida yanayoakisi uwelewa wa Uimamu kuwa unatokana na amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu.”

Akaongeza kuwa “Madhumuni ya wiki ya Imamu awamu ya pili yameakisi falsafa ya maisha na undani wa Aqida ya kuamini Maimamu watakasifu kumi na mbili (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya kupitia wiki ya Imamu huelezea elimu ya Ahlulbait (a.s) na historia yao katika kupambana na changamoto, sambamba na kubainisha nafasi yao (a.s) katika kuondoa shubha na fikra potofu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: