Atabatu Abbasiyya imewapa zawadi wanahabari walioshiriki kutangaza matukio ya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.
Utoaji wa zawadi umefanywa pembezoni mwa hafla ya kufunga wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili iliyosimamiwa na Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kulea mtu na umma) kuanzia tarehe: 27/6/2024m hadi 4/7/2024m.
Zawadi zimekabidhiwa na rais wa kitengo cha habari katika Ataba Sayyid Ali Badri, kutokana na kazi nziru waliyofanya ya kutangaza matukio ya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.
Idara na vituo vya habari wamefanya kazi kubwa ya kutangaza matukio ya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili kupitia vyombo tofauti vya habari.