Jambo hilo analifanya chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kwa lengo la kurahisisha utendaji wa mawakibu na kuangalia mahitaji yao zikiwa zimebaki siku chache kuingia mwezi wa Muharam na ziara ya Ashura.
Muheshimiwa katibu mkuu amefuatana na rais wa maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Ali Muslihu na baadhi ya wawakilishi wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya.
Ataba tukufu hufanya kila iwezalo katika kurahisisha utoaji wa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi wa Muharam na Safar.