Sayyid Swafi amepokea bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amepokea bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya mwezi wa Muharam wa mwaka 1446h, kutoka kwa katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini.

Shughuli ya kupokea bendera imefanywa ndani ya kukumbi wa utawala katika Ataba tukufu, mbele ya makamo katibu mkuu Sayyid Abbasi Mussawi na wajumbe wa kamati kuu.

Atabatu Abbasiyya imeweka bendera zinazoashiria huzuni na majonzi ndani ya haram tukufu na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, kama ishara ya kupokea miezi ya huzuni Muharam na Safar.

Atabatu Abbasiyya imepokea maelfu ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, wanaokuja kushiriki kwenye shughuli ya kubadili bendera ya kubba la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Atabatu Abbasiyya itabadili bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya swala ya Magharibi na Isha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: