Mazingira ya huzuni na majonzi yametanda katika Atabatu Abbasiyya karibu na shughuli ya kubadili bendera ya kubba la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kama tangazo la kuingia kwa mwezi wa Muharam.
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amepokea bendera maalum ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya mwezi wa Muharam wa mwaka 1446h, kutoka kwa katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini.
Atabatu Abbasiyya imeweka bendera zinazoashiria huzuni kwenye haram tukufu na uwanja wa katikati ya haram mbili, kama ishara ya kupokea miezi ya huzuni Muharam na Safar.
Atabatu Abbasiyya imepokea maelfu ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, wanaokuja kushiriki kwenye shughuli ya kubadili bendera za malalo mbili takatifu.
Atabatu wabbasiyya itabadilisha bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya swala ya Magharibi na Isha.