Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amebadilisha bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katoa nyekundu na kuweka nyeusi kama tangazo la kuingia mwezi wa Muharam 1446h.
Shughuli hiyo imeanzia katika Atabatu Husseiniyya, imetolewa bendera nyekundu na kuwekwa nyeusi juu ya kubba la malalo ya Imamu Hussein (a.s), kisha watu wakaelekea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuanza shughuli ya kubadili bendera ya kubba takatifu iliyofanywa kwenye uwanja wa mlango wa Qibla.
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ameshusha bengera nyekundi iliyopo juu ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kupandisha bengera nyeusi inayo ashiria kuanza kwa majonzi na huzuni za Ashura.
Kubadili bendera kutoka nyekungu na kuweka nyeusi ni ishara ya kuingia kwa mwezi wa huzuni, mwezi wa Muharam aliouawa ndani yake Imamu Hussein, ndugu yake Abulfadhil Abbasi, watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.