Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi za kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mhadhiri wa majlisi Shekhe Ali Mujaan amesema “Atabatu Abbasiyya imezowea kufanya majlisi za kuomboleza katika matukio yote ya huzuni mwaka mzima, hususa katika mwezi mtukufu wa Muharam, majlisi huanza saa kumi na mbili na nusu asubuhi, kwa kusimamiwa na mawakibu za waombolezaji ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi usiku, bila kusahau majlisi ambazo hufanywa ndani ya ukumbi wa utawala”.
Akaongeza kuwa “Majlisi ambazo hufanywa katika mwezi wa Muharam hujikita katika kueleza harakati ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akabainisha kuwa “Atabatu Abbasiyya inatoa kipaombele katika kuomboleza mwezi wa Muharam na kuangazia swala la Imamu Hussein kwa kufanya majlisi na harakati tofauti”.