Kupandisha bendera ya huzuni katika nyumba za makazi za Abbasi (a.s).

Nyumba za makazi ya Abbasi (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya, zimeshuhudia shughuli ya kupandisha bendera ya huzuni kama ishara ya kuingia mwezi wa Muharam mwaka 1446h.

Kiongozi wa nyumba hizo Sayyid Haidari Majhuul Muhammad amesema “Imefanyika shughuli ya kupandisha bendera ya huzuni katika nyumba za makazi za Abbasi (a.s), shughuli hiyo imehudhuriwa na wakazi wengi wa nyumba hizo, shughuli ya maombolezo ya Imamu Hussein (a.s) itaendelea”.

Watumishi wa nyumba za makazi wameweka mazingira ya kuomboleza msiba wa Ahlulbait (a.s) kwa kuandaa ratiba yenye vipendele tofauti, ikiwa ni pamoja na kuweka mabango yanayoashiria huzuni kwenye maeneo tofauti ya nyumba, kufanya majlisi za kuomboleza sambamba na kutoa huduma mbalimbali kwa waombolezaji.

Vitengo vyote vya Ataba tukufu hufanya kazi kubwa ya kuweka mazingira ya huzuni na kutoa huduma bora kwa waombolezaji wanaokuja katika malalo mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: