Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kuandaa milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kupokea matembezi ya Towareji.
Makamo rais wa kitengo cha kusimamia haram Sayyid Zainul-Aabidina Quraish amesema “Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vimeanza kuandaa milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kupokea matembezi ya Towareji”.
Akaongeza kuwa “Maandalizi hayo yamehusisha kuweka mchanga laini, kutandika zulia jekundu, kuweka mabango na alama zinazoonyesha milango ya kuingia na kutoka ndani ya haram tukufu”.
Vitengo vya Atabatu Abbasiyya hufanya kila linalowezekana katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mazuwaru wanaokuja kuhuisha Ashura mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka ndani na nje ya taifa.