Idara ya Dini tawi la wanawake inafanya majlisi za kuomboleza za mwezi wa Muharam

Idara ya dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya majlisi za kuomboleza za mwezi wa Muharam.

Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema: “Majlisi hufanywa kila mwaka kuanzia siku ya kwanza hadi ya kumi na tatu ya mwezi wa Muharam katika Sardabu ya Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) ndani ya Ataba tukufu, kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya.

Akaongeza kuwa “Majlisi hufunguliwa kwa Qur’ani tukufu, hufuatiwa na muhadhara wa kidini ambao hutolewa na mmoja wa wahadhiri wa Husseiniyya na huhitimishwa kwa tenzi na qaswida inayotaja masaaibu ya Maimamu (a.s) na yaliyojiri katika siku kama hizi”.

Akaendelea kusema “Majlisi ni sehemu ya harakati za idara ya kuomboleza mwezi wa huzuni, mazuwaru wamezowea kushiriki katika majlisi hizi za kuomboleza”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: