Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imemaliza hatua ya kwanza ya semina ya Qur’ani ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Dini senye asili ya Afrika.
Semina hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.
Semina imeandaa walimu wa Qur’ani tukufu wapatao (18) kutoka nchi tofauti za Afrika.
Nayo ni sehemu ya mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini awamu ya nane, kwa kushirikiana na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Ataba tukufu.
Inaratiba ndefu inayodumu kwa miezi sita, imegawanywa katika awamu kuu tatu, inalenga kujenga uwezo wa washiriki.