Watumishi wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea kuhudumia mazuwaru wa Ataba mbili tukufu katika mji wa Karbala, kupitia maukibu ya Ashbaali-Twafu.
Maukibu hiyo inafanywa kwa mwaka wa nne mfululizo, inagawa maji, juisi na milo miwili ya chakula kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watumishi wa idara ya habari wanafaya kazi kubwa ya kuandaa mahitaji ya kimkakati ya mawakibu, sambamba na kusimamia matangazo, kupokea washiriki wa mawakibu, kugawa chakula cha jioni na kuandaa ratiba ya kila siku yenye vipengele vya Dini, Utamaduni na huduma mbalimbali.
Maukibu inalenga kuwajenga vijana na kuwaongezea maarifa ya Dini yao kupitia ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) na kuwajulisha tukio la Twafu.




