Kwa picha.. Usiku wa mwezi sita Muharam katika mji wa Karbala

Mazuwaru wanahuisha usiku wa mwezi sita Muharam mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala.

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala zimeshuhudia makundi makubwa ya waombolezaji kutoka miji tofauti ya Iraq na ulimwenguni kwa ujumla, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na siku ya mwezi kumi Muharam, siku ambayo waumini huomboleza kifo cha Imamu Hussein, watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Waombolezaji wanahuisha tukio lenye kuumiza, kwa kuenzi misingi ya Imamu Hussein (a.s) na kujitolea kwake katika kutetea haki na uadilifu.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika siku ya Ashura.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: