Amekutana na wanafunzi wa mradi wa kuhifandi Qur’ani unaosimamiwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya.
Rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali amesema “Kukutana na muheshimiwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ni sehemu ya ratiba ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani na kuangalia aina za kuhidhadhi (kawaida, haraka, mazingatio)”.
Akaongeza kuwa “Muheshimiwa katibu mkuu amejikita katika kukagua (kuhifadhi kwa mazingatio), kwani aina hiyo humuwezesha mtu anaehifadhi kufanya mazingatio ya maneno na vitendo”.
Akafafanua kuwa “Katika kikao hicho tumesikiliza nasaha za muheshimiwa katibu mkuu na maelekezo yake yanayolenga kuboresha kiwango cha wanafunzi na kuendelea kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu”.