Mawakibu za watu wa Karbala katika siku ya sita ya mwezi wa Muharam, zimefanya matembezi ya kuomboleza mashahidi wa Twafu.
Barabara zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zimeshuhudia mawakibu nyingi za waombolezaji waliokuwa wakiimba qaswida na tenzi za kusifu msimamo wa wafuasi wa Imamu Hussein waliojitolea kumlinda yeye pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinashuhudia makundi makubwa ya waumini wanaokuja kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), kutoka ndani na nje ya Iraq.
Mawakibu za kuomboleza katika siku kumi za kwanza za mwezi wa Muharam ni maalum kwa wakazi wa Karbala, mawakibu zinaomboleza kwa kufuata utamaduni uliozoeleka toka zamani.
Mawakibu hufuata ratiba iliyoandaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, hupita kwenye barabara maalum zilizoteuliwa hadi kwenye uwanja wa mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huingia katika haram hiyo na kisha hutoka na kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, huhitimisha maombolezo yao mbele ya malalo ya Imamu Hussein (a.s).

















