Maelfu ya mazuwaru wanahuisha usiku wa saba katika mwezi mtukufu wa Muharam

Mazuwaru wanaendelea kuhuisha usiku wa saba katika mwezi wa Muharam mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala.

Makundi makubwa ya waombolezaji kutoka miji tofauti ya Iraq na ulimwenguni kwa ujumla yanamiminika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kujiandaa na siku ya kumi katika mwezi wa Muharam, siku ambayo waislamu huomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Waislamu wamekuwa na utamaduni wa kuomboleza msiba huo mkubwa, kama sehemu ya kumuenzi Imamu Hussein (a.s) na kuelezea kujitolea kwake katika kutetea haki na uadilifu.

Atabatu Abbasiyya inaendelea na ratiba ya kuomboleza na utoaji wa huduma mbalimbali kwa waombolezaji wa kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake katika siku ya Ashura.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: