Majlisi hizo zinasimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu.
Majlisi imefanywa mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.
Idara ya majlisi za kuomboleza imetenga siku ya saba katika mwezi wa Muharam kuwa siku maalum ya kumzungumzia Abulfadhil Abbasi (a.s), historia yake, misimamo yake, kukataa maombi ya madhalimu ya kuanchana na ndugu yake Imamu Hussein (a.s) na mengineyo, mbele ya mahudhurio makubwa ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya Iraq.
Atabatu Abbasiyya hufanya majlisi za kuomboleza katika kipindi chote cha mwaka, hususan siku za mwezi wa Muharam, majlisi huanza saa kumi na mbili asubuhi, sambamba na kusimamia uingiaji na utokaji wa mawakibu za kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi usiku mwingi, bila kusahau majlisi ambazo hufanywa ndani ya ukumbi wa utawala.