Kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya.. Bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imepandishwa katika chuo kikuu cha Misaan.

Chuo kikuu cha Misaan kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu imepandisha bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kama sehemu ya kuhuisha tukio la Twafu.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya Dokta Ahmadi Shekhe Ali amesema “Shughuli ya kupandisha bendera ya huzuni katika chuo cha Misaan, hufanywa siku ya mwezi saba Muharam kwa miaka nane sasa, ukizingatia kuwa siku hiyo ni maalum kwa ajili ya kumuongelea Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya tukio la Twafu”.

Akaongeza kuwa “Shughuli ya kupandisha bendera imehudhuriwa na ujumbe maalum kutoka Atabatu Abbasiyya, walimu wa chuo, viongozi wa hauza na watu wengine wengi, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na surat Fat-ha kwa ajili ya kurehemu waumini”.

Akaendelea kusema “Shughuli hizi ni sehemu ya kukumbuka tukio la Twafu na kueleza yaliyojiri kwa Imamu Hussein, watu wa nyumbani kwake (a.s) na kujitolea kwa ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kupata somo na mazingatio katika tukio hilo, na namna lilivyo linda Dini tukufu ya kiislamu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: