Mazuwaru wanaendelea kuhuisha usiku wa mwezi nane Muharam mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala.
Makundi makubwa ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya Iraq yanaendelea kumiminika katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, kama sehemu ya kujiandaa na siku ya mwezi kumi Muharam, siku ambayo waumini huomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Waumini huomboleza msiba huo mkubwa kwa kuelezea misingi ya Imamu Hussein (a.s) na kujitolea kwake katika kutetea haki na uadilifu.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya uombolezaji na utoaji wa huduma katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) siku ya Ashura.