Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia maukibu ya Ashbaali-Twafu, kimeomboleza kifo cha Qassim mtoto wa Imamu Hassan (a.s) mwezi nane Muharam.
Maukibu ya Ashbaalu-Twafu imeomboleza kifo cha Qassim (a.s) na kuenzi msimamo wake katika haki, wamevaa nguo nyeupe na kuwansha mishumaa huku wakiimba qaswida mashuhuri (Yammi dhakirini min tamri zuffah shabaab).
Kitendo hicho hufanywa kila mwaka na maukibu ya Ashbaalu-Twafu, kina athari kubwa katika nyoyo za vijana.
Maukibu imefanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Husseiniyyuna.. Minal-Mahadi ila llahdi), kwa mwaka wa nne mfululizo, inawashiriki 100 wenye umri wa miaka 7 hadi 12, maombolezo yanadumu kwa muda wa siku kumi, kuanzia mwezi 1 – 10 muharam 1446h.