Huduma mbalimbali zinatolewa na idara ya Zainabiyaat kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Idara ya Zainabiyaat chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, inatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi wa Muharam.

Kiongozi wa idara bibi Susan Ahmadi amesema “Idara inatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kusimamia uingiaji na utokaji ndani ya haram tukufu sambamba na kuweka mazingira tulivu kwa kufanya ibada ya ziara na dua”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wa idara wanasimamia matembezi ya mazuwaru ndani ya haram tukufu, kwa ajili ya kulinda usalama wao na kutoa msaada kulingana na mahitaji yao”.

Idara ya Zainabiyaat inatoa huduma bora kwa wanawake na inaushiriki mkubwa katika matukio ya Dini hususan kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: