Balozi mdogo wa Uturuki katika mkoa wa Najafu, Muheshimiwa Jafari Uljai Karkashi amepongeza huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru katika mwezi wa Muharam.
Ametoa pongezi hizo alipotembelea Ataba tukufu siku ya Jumatatu na kukutana na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Jawadi Hasanawi na rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Ali Azhar na baadhi ya vitengo.
Wameongea kuhusu huduma zinazotolewa kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakati wa ziara zinayohudhuriwa na mamilioni ya watu, hususan katika mwezi wa Muharam na Safar.
Muheshimiwa Karkashi amesema “Huduma zinazotolewa na Ataba tukufu kwa mazuwaru katika mji wa Karbala wakati wa mwezi wa Muharam zinaubora mkubwa kabisa”.
Balozi mdogo wa uturuki Muheshimiwa Jafari Uljai Karkashi na ujumbe aliofuatana nao, wamefanya ziara mbele ya malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).