Mazuwaru wanahuisha usiku wa kumi Muharam mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mjini Karbala.
Makundi makubwa ya waombolezaji kutoka miji tofauti ya Iraq na duniani kwa ujumla, yanakuja Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, kama sehemu ya kujiandaa na siku ya mwezi kumi Muharam, siku ambayo waislamu huomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Waombolezaji wamezowea kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) na kujitolea kwake katika kutetea haki na uadilifu.
Atabatu Abbasiyya inaendelea kutekeleza ratiba ya kuomboleza na kutoa huduma mbalimbali kupitia vitengo vyake, katika kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika siku ya Ashura.