Kitengo cha Dini kinaendelea na majlisi katika mkoa wa Nainawa.

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya majlisi za kuomboleza katika mwezi wa Muharam mkoani Nainawa.

Mmoja wa watumishi wa idara ya maelekezo na msaada chini ya kitengo Shekhe Hamidi Aamiriy amesema “Kitengo cha Dini kinaendelea kufanya majlisi za kuomboleza katika mkoa wa Nainawa kuhuisha mwezi wa Muharam, na kukumbuka kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Idara inafanya majlisi za kuomboleza katika wilaya ya Hamdaniyya mtaa wa Bartwalah, na majlisi zingine zinafanywa katika maeneo tofauti ya mkoa huo”, akasema kuwa “Majlisi zimehusisha ufunguzi wa vituo vya maswali na majibu, kwa lengo la kujibu maswali mbalimbali na kutoa maelekezo ya kidini”.

Akabainisha kuwa “Majlisi zinazofanywa hapa mkoani, zilianza toka siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam na zinaendelea hadi siku ya kumi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: