Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeweka mabango yenye ujumbe elekezi kuhusu ziara ya Ashura.
Mabango yamesanifiwa na watumishi wa kitengo cha habari, uwekaji umesimamiwa na kitengo cha mafundi katika Ataba tukufu.
Mabango yamewekwa sehemu tofauti katika mji wa Karbala na kwenye barabara zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na pembeni mwa barabara ya Jamhuriyya, daraja la Babu Towareji hadi kwenye uwanja mkuu na mbele ya mlango wa qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mabango yameandikwa maelekezo mbalimbali na hadithi za Maimamu (a.s), sambamba na kuonyesha sehemu zinazoweza kuhitajiwa na mazuwaru.