Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anakagua hatua ya mwisho ya maandalizi ya matembezi ya Towareji.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amefanya ziara ndani ya mji wa Karbala kuangalia maandalizi maalum ya matembezi ya Towajeri.

Muheshimiwa katibu mkuu amefuatana na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Muhammad Ashqar, rais wa kitengo cha kulinda nidham Sayyid Hussein Shahristani, kamanda wa kikosi cha kulinda haram mbili tukufu Meja Jenerali Anwaru Abdul-Amiir pamoja na watumishi wa idara ya uhandisi.

Muheshimiwa katibu mkuu amekagua maandalizi ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya katika siku ya Ashura, sambamba na mazingira ya matembezi ya Towareji kwa kuhakikisha kuwa hakuna maafa yatakayo tokea –Allah atuepushie-.

Muheshimiwa katibu mkuu ametembelea pia mawakibu zinazotoa huduma kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: