Majlisi imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo, waumini na mazuwaru waliokuja Atabatu Abbasiyya kutoa pole ya kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) mwezi kumi Muharam, na kuhuisha ahadi ya kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na muhadhara uliojikita katika kueleza msimamo wa Imamu Hussein (a.s), historia yake, kujitolea kwake, na mapambano yake ya kutafuta islahi.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma nai ya kuomboleza iliyotaja tukio la kuuawa kishahidi kwa Abu Abdillahi Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake, katika mazingira yaliyojaa huzuni.
Atabatu Abbasiyya hufanya majlisi Husseiniyya katika kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), na kueleza elimu na utukufu wao (a.s), sambamba na kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).