Marjaa-Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani amelaani kushambuliwa kwa msikiti wa Waadi-Alkabiir katika nchi ya Oman, na kuwapa pole familia za mashahidi.
Ifuatayo ni nakala ya tamko:
Muheshimiwa Sheikh Ihsaan Allawati, Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu, rehema na baraka zake, Allah akuze malipo yetu na malipo yenu kwa kifo cha bwana wa mashidi Abu Abdillahi Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.
Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kushambuliwa kwa waumini waliokuwa wanaomboleza kifo cha bwana wa vijana wa peponi (a.s) ndani ya msikiti katika taifa lenu kipenzi.
Tunalaani shambulio hilo la kigaidi na kuwapa pole familia za mashahidi na waislamu wote kwa ujumla, tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi na kuwaponya haraka majeruhi, adumishe Amani na utulivu katika taifa lunu kipenzi, hakika yeye ni msikivu mwenye kujibu.
Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wameshambuliwa wakati wakifanya maombolezo ya Ashura katika mwezi wa Muharam.

