Kitengo cha utumishi kimeanza hatua ya kwanza ya kusafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya

Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wameanza hatua ya kwanza ya kusafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu na barabara zinazoelekea Ataba.

Wanatoa takataka kwenye barabara na njia zite zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kutumia gari maalum za usafi.

Kazi hiyo imeanza siku ya Alkhamisi mwezi kumi na moja Muharam, baada ya kumaliza ziara ya Ashura na kupokea mawakibu za matembezi ya Towareji.

Ataba tukufu hutumia uwezo wake wote katika kusafisha maeneo yanayozunguka malalo takatifu na kuyafanya kuwa na muonekano mzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: