Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake, nchini Rwanda.
Majlisi imeandaliwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.
Mhadhiri wa majlisi hiyo alikuwa ni Shekhe Haidari Yasi, amefafanua kuwa Imamu Hussein (a.s) alikuwa na msimamo, ametuachia urithi unaotakasa nyoyo na kutupa ujasiri wa kupambana na waovu.
Ametoa muhadhara huo mbele ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s), amehimiza kushikamana na misingi ya Imamu Hussein (a.s), ambapo tunatakiwa kumsoma na kumtambua vilivyo (a.s) ili tuweze kumfanya kiigizo chema katika maisha yetu.