Usomaji wa Qur’ani umefanywa ndani ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) kwa usimamizi wa Maahadi ya Qur’ani chini ya Majaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya.
Katika usomaji huo wameshiriki wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu na kundi kubwa la mazuwaru.
Atanatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake imeandaa ratiba maalum ya uombolezaji na utoaji wa huduma katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein, watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake katika siku ya mwezi kumi Muharam, na siku zingine katika mwezi wa Muharam na Safar.