Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinafanya usafi mkubwa baada ya kukamilika kwa ziara ya Ashura.

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili, kimeanza kusafisha sehemu hiyo baada ya kukamilika kwa maombolezo ya Ashura.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Habibu Dahshi amesema “Watumishi wa kitengo wameanza kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu baada ya kutandua kapeti lekundu, kufuatia kukamilika kwa matembezi ya kuomboleza ya Towareji”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya usafi imehusisha eneo linalozunguka Ataba tukufu, barabara na njia zinazoelekea haram, usafi huo ni sehemu ya kujiandaa na siku ya mwezi kumi na tatu Muharam, na kupokea mawakibu zitakazokuja kufanya kumbukumbu ya kuzikwa miili ya mashahidi wa Karbala”.

Akabainisha kuwa “Watumishi wa kitengo hiki wamefanya kazi kubwa toka siku ya kwanza katika mwezi wa Muharam, wamekuwa wakitoa huduma tofauti kwa waombolezaji waliokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Muharam”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: