Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinajiandaa na ziara ya mwezi kumi na tatu Muharam.

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kinajiandaa na ziara ya mwezi kumi na tatu Muharam, siku ya kukumbuka mazishi ya miili mitakatifu ya Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Muhammad Twawiil amesema “Kitengo kimeweka mkakati maalum wa kupokea waombolezaji wa mwezi kumi na tatu Muharam, siku ya kukumbuka mazishi ya miili mitakatifu ya Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake”.

Akaongeza kuwa “Mkakati unahusisha kuandaa maji baridi ya kunywa na mabarafu, katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili na kwenye barabara zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Wahudumu wa kitengo walianza kazi ya kusafisha uwanja wa katikati wa haram mbili tukufu baada ya kutandua kapeti lekundu na kukamilika kwa matembezi ya Towareji mwezi kumi Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: