Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wanaendelea na kazi ya kusafisha maeneo yanayozunguka Ataba tukufu.
Kazi hiyo inahusisha kuondoa taka zilizopo kwenye barabara zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kutumia mitambo maalum.
Kazi ilianza siku tatu zilizopota, baada ya kukamilika ziara ya Ashura na matembezi ya Towareji.
Wanafanya kazi kubwa ya kusafisha sehemu zote za malalo takatifu na maeneo yanayozunguka eneo hilo.