Majmaa-Ilmi imefanya majlisi ya kumbukumbu ya mazishi ya miili mitakatifu jijini Baghdad

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kumbukumbu ya mazishi ya miili mitukufu jijini Baghdad.

Majlisi imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa.

Majlisi imefanywa kwa kushirikiana na Maukibu ya Thaqalaini na Raabitwatu-Ahlulbait (a.s) katika mji mkuu wa Baghdad, kumbukizi ya mazishi ya miili mitakatifu iliyouawa katika vita ya Twafu.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Haafidh Hussein Alghazi, ikafuatiwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Ali Al-Abusi baada yake zikasomwa qaswida na tenzi kutoka kwa Aqiil Saidi na Haidari Sultani.

Majlisi ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi washiriki kutoka idara ya Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad, kama sehemu ya kuoinyesha thamani ya kazi nzuri wanayofanya ya kuhuisha matukio ya kidini yanayohusu Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: