Kuanza kazi ya kutoa mchanga kwenye milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanafanya kazi ya kuondoa mchanga mbele ya milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kukamilika kwa ziara ya Ashura.

Makamo rais wa kitengo cha kulinda nidham Sayyid Ridhwa Naaji Saahi amesema “Kitengo chetu kwa kushirikiana na vitengo vingine, tunafanya usafi mkubwa kwenye milango ya Ataba, tunatoa michanga yote iliyopo kwenye milango, baada ya kukamilika kwa ziara ya Ashura na matembezi ya Towareji”.

Akaongeza kuwa “Uwekaji wa mchanga kwenye milango ya Atabatu Abbasiyya ulifanywa mwanzoni mwa mwezi wa Muharam, ili kuzuwia mazuwaru wasiteleze na kuanguka wakati wakifanya ziara tukufu, hususan wakati wa matembezi ya Towareji”.

Atabatu Abbasiyya imesafisha kila sehemu ya haram na maeneo yanayozunguka eneo hilo takatifu, na kuyafanya kuwa na muonekano mzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: