Matembezi hayo yamesimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya, ambapo nchi karibu 18 za afrika zimeshiriki.
Kiongozi wa idara ya tablighi katika Markazi, Sayyid Muslim Aljaabiri amesema, “Markazi imeandaa matembezi ya waafrika, yameanzia barabara ya Imamu Zainul-Aabidina hadi malalo ya Imamu Ali (a.s) katika mkoa wa Najafu”.
Akaongeza kuwa “Matembezi yamepewa jina la (Masiirul-Aashiqiin), kwa ajili ya kumpa pole kiongozi wa waumini (a.s), kwa kuuawa mtoto wake Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), sambamba na kuenzi vizito viwili kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu”.
Washiriki wa matembezi hayo, watu wenye asili ya Afrika wamesema “Matembezi yao ni sehemu ya kunusuru Qur’ani tukufu na kuhuisha ahadi ya utiifu kwa kiongozi wa waumini (a.s), na kumpa pole kwa tukio chungu la Twafu”