Kwa watumishi wake.. Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) imefanya warsha kuhusu utendaji wa idara ya kuazimisha

Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imefanya warsha kwa watumishi wake kuhusu utendaji wa idara ya kuazimisha katika Maktaba.

Kiongozi wa Maktaba bibi Nuru Ali amesema “Warsha inalenga kujenga uwezo wa utendaji kwa watumishi, mkufunzi wa warsha hiyo alikuwa ni Ustadhi Abdulhamidi Abduridhwa Ali, kutoka kitengo cha habari na utamaduni katika ofisi ya Daaru-Makhtutwaat ya Ataba, warsha imedumu kwa muda wa siku mbili”.

Akaongeza kuwa “Warsha imejikita katika kufundisha njia za kutambua vitabu vinavyo tafutwa vilivyopo maktaba, sambamba na kufafanua vitengo vyote vya Maktaba na majukumu yake”.

Akaendelea kusema “Katika warsha hiyo pia wamefundishwa namna ya kutumia vifaa vya zima-moto ndani ya maktaba, wamefundishwa kwa nadhariyya na vitendo”.

Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) imekuwa ikiwajengea uwezo watumishi wake kulingana na nafasi zao, ili kuwawezesha kutoa huduma bora zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: