Kikao kimefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Akram Saamir, yakafuata mawaidha kutoka kwa Shekhe Zainul-Aabidina Abayati, ameongea maana ya kujitolea alikofanya Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake.
Akaeleza umuhimu wa kukumbuka misingi ya Imamu Hussein (a.s) na kuifundisha katika nyoyo za waislamu, hususan vijana.
Kikao kimeshuhudia upandishwaji wa bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kikahitimishwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ahmadi Zaalimi.