Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kikao na wataalam wa sekta ya maktaba.
Mkuu wa kituo cha faharasi na upangiliaji wa taaluma chini ya kitengo, Sayyid Hasanain Ahmadi Mussawi amesema “Kituo kinatafuta taarifa mpya katika elimu ya maktaba, ya kisasa zaidi ni (frem – B), kanuni iliyopo katika maktaba na taaluma ya utambuzi, kikao hicho kimehusisha walimu wa sekta ya maktaba kutoka vyuo vikuu vya Italia, Uingereza na Ujerumani”.
Kikao kimehudhuriwa na kundi la walimu, kwa ajili ya kupata taarifa shirikishi na kuziweka kwenye mtandao wa (frem – B) na kuzifanya zionekane kwenye mitandao ya kimataifa kwa lugha ya kiarabu”.
Akafafanua kuwa “Matokeo ya kikao yalikuwa chanya, wataalam wameahidi kutoa taarifa za kiarabu kwenye mitandao kupitia familia ya elimu za maktaba”, akaongeza kuwa “Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma ndio kituo cha kwanza hapa Iraq kujiunga na mfumo huo”.