Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanahuisha siku ya kumi na saba katika mwezi wa Muharam

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamehuisha siku ya kumi na saba katika mwezi wa Muharam kupitia maukibu ya kuomboleza ya pamoja.

Mmoja wa wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Badri Mamitha amesema “Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya huadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s), likiwepo tukio la siku ya kumi na saba katika mwezi wa Muharam”.

Akaongeza kuwa “Maukibu imeanzia ndani ya kumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, huku wakiimba qaswida na mashairi ya kuomboleza, yaliyo amsha hisia za huzuni katika nyoyo za waumini, walipofika katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza”.

Mshauri wa katibu mkuu katika Atabatu Husseiniyya Sayyid Fadhili Auz amesema “Watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wanaendelea kufanya maukibu za kuomboleza matukio yanayo husu Ahlulbait (a.s), maukibu ya leo ni kwa ajili ya kuhuisha siku ya saba toka kuuawa Imamu Hussein (a.s), jambo hili limekuwa likifanywa na Ataba mbili kwa miaka ishiri sasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: