Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kimetangaza kufanikiwa mkakati wa nusu ya kwanza ya mwezi wa Muharam

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa nusu ya kwanza katika mwezi mtukufu wa Muharam.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Muhammad Twawiil amesema “Kitengo kiliandaa mkakati maalum katika nusu ya kwanza ya mwezi wa Muharam, uliohusisha ziara ya Ashura na uombolezaji wa siku ya kumbukumbu ya mazishi ya miili ya Ahlulbait (a.s), ulianza toka siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, ulikuwa na sehemu tatu (Utoaji wa huduma, Ulinzi na usalama, Uratibu)”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimetekeleza majikumu yake kwa kushirikiana na vitengo vingine, ili kuhakikisha huduma bora kwa mazuwaru, mkakati huo ulihusisha kusafisha barabara zinazoelekea kwenye malalo takatifu na uwanja wa katikati ya haram mbili muda wote”.

Kuhusu upande wa uratibu amesema kuwa “Kitengo kimepata mafanikio makubwa, hakujaripotiwa habari mbaya, kazi zote kumefanya kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya toka siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam hadi baada ya kumbukumbu ya kuzikwa miili ya masahahidi wa Twafu, matembezi ya Towareji yamefanywa kwa uratibu na usimamiaji mzuri, wameingia na kutoka salama katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akafafanua kuwa “Kitengo kiliweka watumishi wa idara ya usalama kwenye vituo vyote vya ukaguzi na sehemu mbalimbali, wamefanya kazi kwa ufanisi mkubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: