Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza muhadhara utakaotolewa kwa njia ya mtandao wenye anuani isemayo (haki za watoto).
Muhadhara huo ni sehemu ya mihadhara inayotolewa kwa njia ya mtandao na kituo chini ya anuani isemayo (Mtandao wa elimu katika Risaalatul-Huquqi ya Imamu Sajjaad –a.s-).
Muhadhara utatolewa siku ya Jumamosi (27/7/2024m) saa tano asubuhi.