Awamu ya ishirini na tatu ya hema la mabinti wa Aqida, linalosimamiwa na idara ya shule za Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya, imetoa muhadhara wa kidaktari kwa washiriki.
Muhadhara umetolewa na rais wa kitengo cha madaktari katika Ataba tukufu, Dokta Haifaa Tamimi, ameeleza mambo yanayohusiana na maradhi ya wanawake, njia za kujikinga na tiba zake.
Ametoa maelezo ya kidaktari katika mambo mbalimbali, washiriki wamesema kuwa wamefaidika sana kutokana na muhadhara huo.
Ratiba imehusisha shindano la vikundi lenye anuani isemayo (Pima uwelewa wako) lililoandaliwa na idara ya shule za Alkafeel, lilikuwa na maswali kutoka kwenye maudhui tofauti, kwa ajili ya kujenga moyo wa ushindani kwa washiriki.
Hema la mabinti wa Aqida ni hatua muhimu katika juhudi za Atabatu Abbasiyya, katika kujenga uwelewa wa Dini na Utamaduni kwa wanafunzi wa vyuo, na kuwaandaa kuwa na ushiriki mzuri katika jamii.