Muheshimiwa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, amesisitiza umuhimu wa usafi katika ziara ya Arubaini.
Amesema hayo wakati alipojibu maswali kutoka kwa waumini tarehe tatu Safar mwaka 1438 hijitiyya, kuhusu namna ya kuamiliana na uchafu, uratibu wa Mawakibu Husseiniyya na njia bora ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s).
Alisisitiza kuwa kujitolea mali kwa ajili ya kununua mifuko na pipa za kutupia taka, sambamba na kujitolea kufanya usafi ni miongoni mwa mambo mazuri kisheria, kufanya hivyo pia ni sehemu ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s).
Ametahadharisha utupaji wa mabaki ya vyakula pembeni ya barabara, akasema jumbo hilo halifai kisheria kwani linaudhi watumiaji wa barabara pia ni sehemu ya kusambaza uchafu.
Muheshimiwa Sayyid Sistani ametoa wito kwa Mawakibu Husseiniyya zote kudumisha usafi, akasema kudumisha usafi ni sehemu ya adabu za Zaairu.
Akasisitiza kuwa usafi ni sunna kisheria na unachangia kufanikisha ziara tukufu ya Arubaini.