Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, ameshiriki kwenye kazi ya kusafisha na kupuliza marashi pamoja na watumishi wengine wa Ataba tukufu.
Rais wa kitengo cha kusimamia haram tukufu Sayyid Khaliil Mahadi Hanuun amesema “Kazi tuliyofanya ndani ya haram tukufu, imehusisha kusafisha na kupuliza marashi kwa kutumia vifaa maalum, ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na ziara ya Arubaini”.
Akaongeza kuwa “Kazi imehusisha kuteua milango maalum ndani ya haram, ambayo imewekwa vitenganishi, kuweka vitabu vya dua na ziara kwenye kabati za vitabu, kwa lengo la kujiandaa na mazuwaru wa mwezi wa Muharam na Safar”.
Vitengo vyote vya Ataba vinafanya maandalizi makubwa, kutokana na kukaribia ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ambayo hufanywa tarehe ishirini ya mwezi wa Safar.